Habari

Serikali yapanga kuwasilisha muswaada ambao utawezesha watoto wote kufaidi sera ya elimu bure

Serikali imepanga kuwasilisha muswada wa sheria bungeni utakaohakikisha watoto wote wanaosoma shule za msingi na sekondari hawatasitisha masomo yao kutokana na ndoa za utotoni.

HaRRISON MWAKYEMBEE

Waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe, amesema hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Ileje, Mhe. Janeth Mbene aliyetaka kujua ni lini serikali itafanya marekebisho wa sheria ya ndoa hizo nchini.

Waziri Mwakyembe amesema kuwa mswada huo utaleta mabadiliko makubwa katika sheria ya elimu ambapo inataka kila mtoto aweze kufaidi sera ya elimu bure.

Hata hivyo, Wizara pamoja na tume ya kurekebisha sheria imepanga kufanya zoezi la kukusanya maoni kuhusu sheria nyingine za wanawake kwa kuwafikia wanawake wengi zaidi kwa kutumia mfumo wa White paper.

Dkt. Mwakyembe aliongezea kuwa kutokana na mchakato wa kuundwa kwa tume ya mabadiliko ya Katiba mpya, mchakato wa kufanya marekebisho ya sheria ya ndoa na mapendekezo ya kutungwa kwa sheria mpya ya mirathi na urithi ulisitishwa kwa muda ili kupisha ukusanyani wa maoni ya katiba mpya.

Baada ya tume ya mabadiliko ya katiba kukamilisha kazi yake imebainika kuwa maoni ya wananchi hayakujielekeza kwenye maudhia ya sheria ya ndoa na sheria ya mirathi ambapo amesema serikali imeanza mchakato wa kuendelea na taratibu za kutungwa kwa sheria hizo, alifafanua Waziri Mwakyembe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents