Habari

Serikali yavipiga kufuli viwanda viwili na kuvitoza faini

Serikali imevifungia na kuvitoza faini viwanda viwili vya kuponda kokoto jumla ya shilingi milioni 4 na laki 5 kwa makosa mbalimbali ikiwemo la ukiukaji wa sheria ya usalama mahali pa kazi.

1-4
Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira,Mhe Anthony Mavunde.

Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira,Mhe Anthony Mavunde amevifungia viwanda hivyo vilivyopo wilayani Bahi mkoani Dodoma baada ya kufanya ziara ya kushtukiza na kubainika wafanyakazi wake kutokuwa na vifaa vya kujikinga kutokana na uchafu wa mazingira.

Aidha waziri Mavunde aligundua katika viwanda hivyo kuna viongozi wa kigeni ambao wapo nchini Tanzania bila vibali huku akiagiza ofisi ya uhamiaji na kuwachukulia hatua.

“Tumegundua kwamba asilimia kubwa ya wafanyakazi hawa wa kigeni wapo nchini kinyume cha utaratibu,wengi hawana vibali vya kazi na nimeshaagiza mamlaka kuja kuwachukulia hatua hasa wenzetu wa uhamiaji pamoja na ofisi yetu watalifanyia kazi hilo,”alisema Mavunde.

“Kwahiyo tumewatoza faini ya shilingi milioni 4 na laki 5 na tunataka walipe ndani ya siku 30 lakini wakati huo huo shughuli zote hazitaendelea za baadhi ya mitambo hapo mpaka pale watakapokuwa wamerekebisha masuala yote,” aliongeza.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents