Burudani

Shughuli ya kimila kuwapeleka Babu Seya na Papii Kocha Congo

Wasanii wa muziki wa dansi, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ wanatarajia kwenda kwao nchini Congo kwa ajili ya shughuli ya kimila.

Msanii Kikumba Mpango ‘King Kikii’ ambaye ni mtu wa karibu wa wasanii hao amekiambia kituo cha Runinga cha Azam kuwa Babu Seya na Papii Kocha wataenda nyumbani kwa ajili kutembelea kaburi la mama yao mzazi.

“Hawa watu, Nguza na mwanawe inatakiwa kwanza baada ya mapumziko inatakiwa wafunge safari waendee nyumbani (Congo), unajua mama Nguza alikuwepo hapa wakati alikuwa hai alikuwa anamuona mwanaye lakini alikuwa ameshakata tamaa kwa bahati mbaya akaenda nyumbani kufika na yeye akafariki,” amesema.

“Sasa kimila inatakiwa wafike kwanza, wafike mpaka kwenye kaburi ya mama mzazi, kabla ya yeye kufanya kitu chochote halafu baada hapo ndio mambo mengine yatafuata,” ameongeza.

Babu Seya na Papii Kocha walitoka gerezani December 9 mwaka huu walipokuwa wakitumikia kifungo cha maisha mara baada ya kupata msamaha wa Rais Dkt. John Magufuli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents