Michezo

Simba itacheza na bingwa wa Afrika Kusini – Manara (Video)

Klabu ya Simba ambayo ipo kambini huko nchini Afrika Kusini ikijiweka sawa kwaajili ya msimu mpya wa ligi kuu na mashindano mbali mbali inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika Kusini, Bidvest Wits siku ya Alhamisi ya wiki hii.

Baadhi ya wachezaji wa Simba wakiwa katika mazoezi nchini Afrika Kusini

Msemaji wa Simba SC, Haji Manara amethibitisha hilo huku akitoa ratiba nzima ya michezo ya kirafiki itakayocheza timu hiyo

“Siku ya Alhamisi Simba inatarajiwa kucheza na mabingwa wa Afrika Kusini timu ya Bidvest Wits pale Johannesburg na tayari baadhi ya wachezaji wetu muhimu wameshajiunga na timu wako wachache ambao wanatarajia kujiunga wikiendi hii”.Amesema Manara

“Katika mechi ya Simba Day klabu yetu inatarajia kucheza na mabingwa wa Rwanda FC Rayon Agosti 8 tunatarajiwa kwamba maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu wajitokeze hususan ni mashabiki wa Simba wajitokeze siku hiyo pamoja na mbo mengine ya utambulisho wa Jezi na Wachezaji wapya laikini safari hii ni maalumu zaidi hasa kutokana na usajili na maandalizi yaliyofanywa ukizingatia kikosi kipo kambi nje ya nchi” .

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents