Simba Wamtaka Ghost Mulee

Uongozi wa klabu ya Simba umeanza kufanya mazungumzo na aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Tusker ya Kenya, Jacob `Ghost` Mulee ili aweze kuchukua nafasi ya Mbulgaria, Krasimir Bezinski, ambaye anatazamiwa kuondoka kurejea kwao.

Uongozi wa klabu ya Simba umeanza kufanya mazungumzo na aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Tusker ya Kenya, Jacob `Ghost` Mulee ili aweze kuchukua nafasi ya Mbulgaria, Krasimir Bezinski, ambaye anatazamiwa kuondoka kurejea kwao.

Akizungumza na Nipashe jana kwa njia ya simu, Mulee alisema kuwa mmoja wa viongozi wa Simba (jina tunalo) amekuwa akimpigia simu mara kwa mara na kumueleza nia yao ya kutaka aje nchini kuifundisha Simba na kuwaambia kuwa bado anajifikiria.

Mulee alisema kuwa mara baada ya kufukuzwa na uongozi wa Tusker aliamua kupeleka nguvu zake katika kituo chake cha watoto na hivyo ameshindwa kuwapa jibu kuwa kama ataweza kuja kujiunga na Simba.

“….amenipigia simu na kunitaka nije Dar es Salaam kwa ajili ya kuifundisha Simba, amenieleza jinsi timu ilivyofanya vibaya katika mechi za ligi,“ alisema Mulee.

Aliongeza kuwa sababu ambayo inamfanya ashindwe kutoa maamuzi ya haraka ni kutokana na uongozi wa timu za nchi za Afrika Mashariki, kupenda kuingilia kazi ya kocha na pale timu inapofanya vibaya lawama huwa kwa kocha na sifa kuharibika.

Alisema kuwa licha ya mambo hayo pia fedha, ambazo viongozi hao wanataka kumlipa ni ndogo ukilinganisha na zile, ambazo wanawapa makocha kutoka nchi za Ulaya.

“Wanapenda kutushushia thamani sisi makocha weusi na kuona wazungu ndio wana thamani, hili pia ni jambo ninalolifikiria kabla ya kuchukua uamuzi wa mwisho,“ aliongeza kocha huyo ambaye aliwahi kuipa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati klabu ya APR ya Rwanda mara mbili mfululizo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents