AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Simba yakubali kipigo cha aibu kutoka kwa TP Mazembe

Timu ya Simba SC ya nchini Tanzania imekubali kipigo kizito cha goli 4 kwa moja kutoka kwa mabingwa mara 4 wa CAF Champions League, klabu ya TP Mazembe.

Simba walianza kupata goli lao la kwanza dakika ya 2 kupitia Okwi baada ya kupokea pasi matata kutoka kwa Haruna Niyonzima ambaye dakika za mwanzo alionekana kucheza vizuri katika nafasi ya kiungo.

Kuanzia dakika ya 23 TP Mazembe alianza kuamka na kufanikiwa kupata goli lao la kwanza kupitia Kabaso Chongo. Mvua ya magoli iliendelea mpaka kufika dakika ya 75 tayari klabu hiyo yenye makazi yake Lubumbashi ilikuwa imepata goli nne.

Klabu ya Simba ambayo kwa sasa inashika nafasi ya tatu Ligi Kuu Tanzania Bara, ina rekodi mbaya kwa michezo ya nje katika mashindano ya CAF Champions League , kwani katika michezo minne ya ugenini amefungwa magoli 16.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW