DStv Inogilee!

Simeone amvulia kofia Cristiano Ronaldo baada ya kupiga Hat Trick

Hat Trick ya Cristiano Ronaldo imeipeleka klabu ya Juventus hatua ya Robo fainali Ligi ya Mabingwa baada ya kuifunga Atletico Madrid mabao 3-0 jana Jumanne usiku kwenye Uwanja wa Allianz katika mchezo wa marudio.

Mabao ya Ronaldo yaliwekwa wavuni dakika za 27, 48 na 86 na kuwafanya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2 ambapo mechi yao ya awali Juventus walilimwa mabao 2-0.

Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri alimsifu Ronaldo kwa kiwango alichokionyesha mchezo wa jana huku akisema ulikuwa ni mchezo wa kuvutia.

Upande wa Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone alisema Ronaldo ni mchezaji bora wa dunia, ameonyesha kiwango cha tofauti usiku wa jana.

Alikumbushia kuwa ameonyesha kiwango ambacho amewahi kucheza yeye enzi zake na jambo la kipekee ameweza kuonyesha ubora wake.

Juventus imeungana na timu za Manchester City, Ajax, Porto na Tottenham Hotspur kwenye hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Leo Jumatano usiku itapigwa michezo mingine ambapo Liverpool wataonyesha umwamba na Bayern Mnich na Barcelona watawakaribisha Lyon.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW