Habari

Spika wa Bunge aweka wazi siku ya kuapishwa Rais mpya Zimbabwe

Baada ya Spika wa Bunge la nchini Zimbabwe, Jacob Mudenda Jumanne hii kutangaza kujiuzulu kwa Rais Robert Gabriel Mugabe, ameweka tena wazi siku ya kuapishwa kwa kiongozi mpya atakayekalia kiti hicho kilichoachwa wazi.


Robert Mugabe akiwa na Emmerson Mnangagwa

Kwa mujibu wa shirika la habari la ZBC la Zimbabwe, Spika Mudenda amezugumza na waandishi wa habari katika jengo la Bunge mchana huu na kusema, kwa mujibu wa katiba wa chama cha Zanu-PF kimemteua makamu wa rais wa zamani Emmerson Mnangagwa kuchukua nafasi ya Robert Mugabe kama rais wa Jamhuri ya Zimbabwe.

Spika Mudenda ameongeza, Bunge limemwambia Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais na Baraza la Mawaziri, Dk Misheck Sibanda kuteuliwa kwa Mnangagwa ili afanye maandalizi ya sherehe ya kuapa kwake kama rais wa Zimbabwe.

Spika huyo amesisitiza kuwa Dr Sibanda anafanya mipango ya kuhakikisha kiapo hiko kinafanyika siku ya Ijumaa hii.

Mnangagwa anatarajiwa kuwasili leo nchini Zimbabwe ambapo atatua katika uwanja wa ndege wa Manyame Airbase uliopo mjini Harare akitokea huko alipokuwa amekimbilia baada ya kufutwa kazi na Rais Mugabe wiki mbili zilizopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents