Michezo

Staili ya vidole vya Manara vyaikera Yanga (Video)

Uongozi wa klabu ya Yanga umetoataarifa ya kusikitishwa na kitendo cha taasisi ya Bodi ya Ligi , Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadhamini wakuu wa ligi hiyo Vodacom kwa kitendo cha kukabidhi vifaa kwaajili ya msimu mpya bila ya kushirikishwa.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu hiyo, Salum Mkemi

Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu hiyo, Salum Mkemi ambapo amesema jambo hilo limeonyesha dharau kubwa kwa viongozi.

“Bodi ya Ligi , Shirikisho la soka Tanzania (TFF) na wadhamini wakuu wa ligi Vodacom, klabu ya Yanga imesikitishwa na kitendo walichokifanya tukio kubwa la kukabidhi vifaa vya msimu mpya wa 2017/18 bila ya kutushirikisha kitendo ambacho sichakiungwana, kimetudhalilisha, viongozi,wanachama, wapenzi na mashabikiwote wa Yanga” amesema Salum Mkemi

Msemaji wa klabu ya Simba,Haji Manara (katikati) akiwa ameinua vidole juu huku akiwa anaiwakilisha Yanga katika ugawaji wa Jezi 

Mkemi ameongeza kuwa “Yanga ninani katika timu za Tanzania, Dar es salaam Young Africa iakumbukwakuwa ndiyo bingwa mtetezi wa ligi ya Vodacom ikitetea kombe hilo kwa kunyakuwa mara tatu mfululizo,ikilichukua mara nne ndani ya miaka mitano na tumelichukua kombe hilo mara saba ndani ya miaka kumi tazama thamani ya Yanga”

“Nini kifanyike kwa taasisi hizi, tumewaomba TFF, Bodi ya Ligi,Vodacom Tanzania zituandikie maandishi ya kutuomba radhi na kutusafisha na kashifa ya kutoudhuria tukio la kugawa vifaa vya msimu wa 2017/18 tukio ambalo hawakutualika na kuwapa nfasi wapinzani wetu kutambulisha jezi zetu kwa niaba yetu”

 “Vodacom hawajanunua jezi za Yanga za msimu wa 2017/18 hizo sisi tumepewa na Sportpesa na nimali halisi ya Dar es salaam Young Africans  kwa kifupi hawajatununulia chochote katika hizo Jezi, watuombe radhi kwamaandishi na wadhamini wetu”

 By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents