Stars yawapa raha Watanzania

Stars yawapa raha Watanzania
Timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa
Stars jana iliweza kumaliza machungu ya mashabiki wa soka nchini baada
ya kuilaza New Zealand 2-1 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye
Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam

Shujaa wa Stars, alikuwa kiungo wa JKT Ruvu, Moshi Kazimoto baada ya kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Mussa Hassan `Mgosi’.

Wachezaji hao wote waliingia katika
kipindi cha pili kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na Kocha wa Stars,
Marcio Maximo na kuongeza uhai katika timu hiyo.

Kwa hakika Stars isingeibuka na ushini katika mchezo huo, ingebidi wajilaumu kutokana na kukosa nafasi nyingi za wazi.

Pamoja na ushindi huo, Stars kwa kiasi
kikubwa ni wazi inakabiliwa na tatizo la ubutu katika safu yake ya
ushambuliaji, jambo linalotakiwa kutiliwa mkazo na Maximo wakati huu
akiwa `bize’ kuisuka upya timu hiyo kwa ajili ya siku za usoni.

Mrisho Ngassa, Jerry Tegete na John Boko
ndio itabidi wajilaumu zaidi kutokana na kupoteza nafasi kibao dhidi ya
mabingwa hao wa ukanda wa Oceania.

Stars walianza kwa kishindo mchezo huo,
hata hivyo, ilipoteza nafasi nzuri ya kupata bao mapema dakika ya pili
lakini wakati Ngassa alipozuiwa na beki wa New Zealand, Tony Lockehead.

New Zealand, ilijibu shambulizi hilo na
kuweza kupata kona iliyopelekea bao katika dakika ya 11 lilipopatikana
kwa penati iliyofungwa na Shane Smeltz.

Mwamuzi Oden Mbaga alitoa penati hiyo baada ya kiungo wa Stars, Shabaan Nditi kuunawa mpira wakati akiokoa mpira wa kona.

Hata hivyo, ilipoteza nafasi nzuri ya kupata bao mapema dakika ya pili lakini akazuiwa na beki wa New Zealand, Tony Lockehead.

Ngassa aliipotezea Stars nafasi ya
kusawazisha katika dakika ya 27 akiwa na kipa na kupiga shuti ambapo
Tegete naye alishindwa kuzamisha wavuni wakati akiwa na goli tupu na
kuingia mwenyewe wavuni.

Stars iliingia kwa nguvu zaidi katika
kipindi cha pili na kuishambulia vikali New Zealand, ambayo wachezaji
wake walionekana kuchoka baada ya kuisumbua Stars katika kipindi cha
kwanza Ngassa aliweza kusawazisha makosa yake ya kushindwa kujaza
mipira kadhaa wavuni kwa kusababisha bao la Stars la kusawazisha baada
ya kupokea pasi ya Henry Joseph katika dakika ya 58.

Alipiga shuti la mbali lililombabatiza
Tegete aliyekuwa anaonekena ameotea kiasi cha kusababisha malalamiko
kutoka kwa New Zealand.

Bao hilo liliwapa nguvu zaidi Stars na
kuzidi kuwabana New Zealand na Kazimoto akazamisha bao la ushindi
dakika moja kabla ya mpira kumalizika.

Boko alipoteza nafasi za wazi za kuzamisha bao katika dakika ya 75 alipiga nje na kwenye dakika za majeruhi, akapaisha mpira.

Maximo aliwamwagia sifa, ambao hawakupewa nafasi na kuridhika na kiwango chao cha mchezo na kucheza kwa ari.

Kocha wa New Zealand, Hurbeth Ricki
ameisifia Stars na kueleza wachezaji wake wengi hawakuwa wa kikosi cha
kwanza na aliwapa nafasi ya kucheza ili waweze kuelewana.

Timu zilikuwa:

Taifa Stars;Shabaan Dihile, Erasto
Nyoni, Juma Jabu, Salum Sued, Nadir Haroub `Cannavaro’, Shabaan Nditi,
Mrisho Ngassa, Henry Joseph(John Boko dk.82), Jerry Tegete, Nizar
Khalfan (Moshi Kazimoto dk.46) na Kiggi Makassy (Mussa Hassan `Mgosi’
dk.70).

New Zealand:Mark Paston. David Muligan,
Steven Old, Tony Lockhead, Leo Bertos, Tim Brown, Jeremy Christie,
Jeremy Brockie(Andy Barron dk.70), Shane Smeltz(Chris James dk.75),
Chris Wood na Ivan Vicilich.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents