Supa Pesa yatoa milioni 10

Mshindi wa kwanza wa millioni kumi wa bahati nasibu ya kipekee ya SUPA PESA ametokea Mtoni kwa Azizi Ali jijini Dar es Salaam. Mfanyabiashara Khamis Mohamed Khamis amejinyakulia kitita cha milioni kumi ijumaa iliyopita kwenye droo ya wiki ya Supa Pesa.

Bwana Khamis ambaye ana familia yenye watoto watatu amefurahishwa sana na ushindi wake na kusema “Kweli nilidhani ni kama utani nilipopigiwa simu kujulishwa kuwa nimeshinda shilingi milioni 10 na Supa Pesa! Nimelala masikini nimeamka tajiri! Niliona matangazo ya bahati nasibu hii kwenye gazeti na nikaagiza vocha kujaribu kushiriki. Sikutegemea kushinda kwa kweli na hata kama nilitegemea ushindi milioni kumi haikuwa mawazoni kwangu”.

“Nitatumia fedha hizi kufungua account bank na kuimarisha familia yangu ambayo sasa  itakuwa na uhakika wa kotukuwa na matatizo madogo madogo ya kifedha. Na vile vile nitaziwekeza kwenye biashara yangu ili iendelee kukua. Nimefurahi sana, watanzania chezeni bahati nasibu ya Supa Pesa kwani ushindi ni wazi wazi.”

Mfanyabiashara huyu anahusika na biashara ya vifaa vya ujenzi na amesisitiza kuwa hataishia hapa, ataendelea kushiriki na supa pesa zaidi na zaidi.

Msemaji wa Supa Pesa Bi. Nancy Sumari kwenye tarija ya kukabidhi hundi ya mshindi alisema “kila siku washindi watatu wanajinyakulia shilingi milioni moja. Na mpaka sasa washindi wametoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kama Arusha, Tanga, Shinyanga, Dar es Salaam, Mbeya na Kilimanjaro. Ni mchezo rahisi sana kushiriki kwani mtandao wowote unafaa na haichukui muda mwingi wala pesa nyingi. Tuma ujumbe wako sasa andika neno SUPA kwenda 15777 na ufaidi matunda ya Supa Pesa”.

Bahati nasibu hii inahusisha mitandao ya Zain, Tigo, Zantel na Vodacom kwa shilingi 500 tu bila VAT.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents