Habari

Taarifa za kuaga mwili na mazishi ya Profesa Maji Marefu, Mtoto wake aeleza

Aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Steven Ngonyani maarufu kama Profesa Maji Marefu,ataagwa kesho kuanzia saa tatu kwa jiji la Dar es Salaam na baadaye mwili kusafirishwa kuelekea jimboni kwake Korogwe kwaajili ya mazishi.

Akiongea na Bongo5, Mtoto wa Marehemu Thomas Stephen (Profesa Maji marefu) amesema kuwa kwasasa wanasubiri taarifa kutoka serikalini sehemu atakayo agwa kwa Dar es Salaam.

“Kwa Dar es Salaam ataagwa kesho saa tatu na kuhusu ataagiwa wapi tunasubiri taarifa kutoka serikalini,” amesema Thomas.

Prof. Maji Marefu amefariki jana, Juni 2, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alipokuwa akipatiwa matibabu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents