Michezo

Taarifa za usajili barani ulaya Jumatatu hii, Silva, Lennon, Krkic, Diaz, Balotelli, Silva na wengine sokoni

Mshambuliaji wa Marseille Mario Balotelli, 28, anasema kuwa anataka kumaliza kazi yake ya kusakata soka kwa kuichezea timu yake ya nyumbani ya Brescia nchini Itali. (goal)

Mkufunzi wa Everton Marco Silva anasema kuwa anajua kwamba yuko chini ya shinikizo baada ya kikosi chake kushindwa na klabu ya Wolves na kusalia katika nafasi ya tisa katika jedwali la ligi ya Uingereza. (mirror)

Klabu ya Leeds inataka kumnunua winga wake wa zamani Aaron lennon, 31, kurudi katika klabu hiyo kwa kupitia kumsajili kutoka klabu ya Burnley mwisho wa msimu huu. (sun)

Mshambuliaji wa Stoke City Bojan Krkic ,28, huenda akahamia katika klabu ya ligi ya Marekani New England Revolution ambayo imejitolea kumlipa mara mbili marupurupu yake huku dirisha la uhamisho nchini Marekani likiendelea kuwa wazi hadi tarehe mosi mwezi Mei. (sun)

Real Madrid haitamuuza kwa mkopo mwisho wa msimu huu kiungo wa kati wa Uhispania mwenye umri wa miaka 19 kinda Ibrahim Diaz ambaye walimsajili kutoka Manchester City. (AS)

Shirikisho la soka la Uingereza FA linataka kuanzisha refa wa kwanza atakayesimamia mechi za ligi ya wanawake ya.. (telegraph).

Kiungo wa kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21, huenda akaitwa na timu ya Uingereza ilio na wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 baada ya kushirikishwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.(Chronicle).

Kipa wa Real Madrid Thibaut Courtois angependelea kwamba klabu hiyo ingemsaini mshambuliaji wa Ubelgiji na Chelsea Eden Hazard, 28, badala ya raia wa Brazil na Paris St-Germain Neymar, 26. (Het Nieuwsblad, via Sun on Sunday)

Chelsea huenda ikaipatia upinzani Manchester United kwa kumwania mkufunzi wa Tottenham Mauricio mwisho wa msimu huu . (Sunday Express)

Juventus inataka kumsajili upya kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 25, na kumchezesha raia huyo wa Ufaransa na kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey . Klabu hiyo ya Itali inatarajiwa kumsajili Ramsey wakati kandarasi yake itakapokamilika msimu huu. (iBancoNero, via Sunday Mirror)

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anataka kumsaini beki wa Leicester na Uingereza Ben Chilwell, 22, na beki wa Crystal Palace anayecheza katika timu isiozidi miaka 21 Aaron Wan-Bissaka, 21, mwisho wa msimu huu. (Sun on Sunday)

Kaimu mkufunzi wa klabu ya Man United Ole Gunnar Solskjaer anamtaka kipa wa Uhispania David de Gea, 28, kufuata nyayo za mshambuliaji Anthony Martial, 23, kwa kutia saini kandarasi mpya . (Evening Standard)

Bayern Munich tayari inataka kutoa dau la £45m kumnunua mshambuliaji wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, 18. (Sun on Sunday)

Tottenham inajiandaa kutoa kitita cha £50m ili kumnunua kiungo wa kati wa Bournemouth na Wales David Brooks mwisho wa msimu huu , huku Man United ikiwa miongoni mwa klabu zinazomwinda mchezaji huyo 21. (Sunday Mirror)

Tottenham walikuwa tayari kukubali kumnunua mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Michy Batshuayi lakini ‘the Blues’ walipinga uamuzi huo kwa kuwa hawakutaka kuwaimarisha wapinzani wao. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na Crystal Palace badala yake. . (DH, via Sun on Sunday)

Arsenal inaamini kwamba wao ndio wenye uwezo wa kumsajili kiungo wa kati wa Paris St-Germain na Ufaransa Adrien Rabiot, 23, ambaye atapatikana kwa uhamisho wa bila malipo mwisho wa msimu huu (Sunday Mirror)

Mmiliki wa klabu ya Newcastle United Mike Ashley anatarajia kwamba mkufunzi Rafael Benitez, ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa msimu huu atatia saini kandarsi mpya katika klabu hiyo kufuatia kusajiliwa kwa kiungo wakati wa Paraguay Miguel Almiron, 24. (Sunday Mirror)

Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez anasema kuwa winga Jacob Murphy bado anathaminiwa katika klabu ya Newcastle, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kujiunga na West Brom kwa mkopo wa kipindi chote cha msimu kilichosalia. (Chronicle)

Kiungo wa kati wa PSG Marco Verratti huenda akaimarika kwa mkondo wa kwanza wa mechi ya vilabu bingwa raundi ya muondoano dhidi ya Manchester United siku ya Jumanne 12 Februari. (Mail on Sunday)

Kiungo wa kati wa Arsenal Emile Smith-Rowe, 18, amejiunga na klabu ya RB Leipzig kwa mkopo mnamo mwezi Januari lakini hatoweza kuanza kuichezea miamba hiyo ya Ujerumani kwa kipindi cha wiki tatu kutokana na jeraha la nyonga. . (Independent on Sunday)

Chanzo bbc

By Ally Juma.


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents