Habari

TAKUKURU yamuonya Mh. Nassari, ‘Hii Taasisi haishinikizwi’

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (Takukuru) imetoa onyo kwa Mbuge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Mhe. Joshua Nassari kwa kushinikiza kuchukulia hatua za haraka kwa kile anachokiita ushahidi wa madiwani wa chama hicho Arusha waliojitoa kwa madai ya srushwa.

Akizungumza Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa TAKUKURU, Valentino Mlowola amemtaka Nassari na mbunge mwenzake wa Arusha Mjini Godbless Lema kuwa na subira na kutokishinikiza chombo hicho kuchukua hatua haraka na kutoingiza suala hilo katika siasa.

“Namuonya Mhe. Nassari ameshaleta taarifa yake kwetu atuachie tuyafanyie kazi yale yanayotupasa kufanya kwa mujibu wa sheria na siyo kutushinikiza kama kauli aliyotoa jana, hii taasisi haishinikizwi na mtu yeyote, ukiangalia sheria tuko huru kufanya majukumu yetu” amesema.

“Endapo ataendelea na utaratibu huu afuate sheria na tutachukua hatua za kisheria dhidi yake bila kuathiri nafasi ya taarifa aliyotupatia ambayo tunaifanyia kazi” ameongeza.

Katika hatua nyingine amesema kuwa wananchi wanaotaka kuipatia taasisi hiyo taarifa wapo tayari kuzipokea  lakini wazingatie matakwa ya kisheria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents