Burudani

Tamaa mbaya: Parker anataka kulipwa fidia baada ya ugomvi wa Chris Brown na Drake!


Uongozi wa klabu ya usiku ya W.i.P. ya New York unasema ni ujinga kwa Tony Parker kuishtaki klabu hiyo kutokana na ugomvi wa Chris Brown na Drake na kusema kuwa hakuna jinsi wangeweza kutabiri kile kilichotokea.

Alhamis hii Parker amefungua kesi ya madai ya kutaka alipwe dola milioni 20 na klabu hiyo kwa madai kuwa klabu hiyo ilitakiwa kufahamu Drake na Chris hawapatani na badala yake iliwachochea kwa kuwauizia pombe. Mtandao wa TMZ unasema, klabu hiyo inaona kuwa ugomvi huo ulikuwa nje ya uwezo wake na walifanya kila waliloweza kuuzima ugomvi huo haraka iwezakanavyo.

Vyanzo vya mtandao huo vimesema klabu hiyo inaziona shutuma za Parker kama za kipuuzi na kusema kuwa walikuwa na walinzi zaidi ya 15 wakilinda klabu usiku huo na wamiliki hawachagui nani aingie ama nani asiingie. Parker aliyekuwepo kwenye klabu hiyo wakati ugomvi unaendelea anasema alijeruhiwa na hivyo anataka alipwe fidia.

Kijana huyo ambaye alizaliwa kwa jina la William Anthony Parker Jr ni mchezaji wa kulipwa wa mpira wa kikapu katika timu ya NBA ya San Antonio Spurs.

Parker pia alikuwa mume wa muigizaji maarufu Eva Longoria.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents