Habari

Tanesco yaanza kukata umeme kwa wadaiwa sugu. Polisi na Hospitali zimo.

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limeanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli la kuanza kukata umeme katika baadhi ya Taasisi za serikali zinazodaiwa na shirika hilo kwa kuanza na vituo vya polisi 13, maduka ya Jeshi na hospitali za serikali, kutokana na malimbikizo ya madeni zaidi ya shilingi bilioni 8.

Akizungumza kwa niaba ya Meneja wa Tanesco Mkoani Arusha, Ofisa Uhusiano wa Tanesco mkoani hapo, Saidi Mremi amesema zoezi hilo limefanyika ikiwa ni hatua ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Magufuli ili kuweza kukusanya madeni.

“Tumepita vituo kama vya polisi pamoja na vya Jeshi, tumepita cenral polisi hapa mkoani, tumepita pia kwa RPC tumekata umeme, kwa traffic polisi tumekata umeme, vituo vya polisi kama unga limited,Ngarenaro, Sakina,Ngaramtoni,Sekei, Fire, Kijenge, Chekereni, Olorien na Mbauda hivi ndivyo vituo vya polisi ambavyo tumevikatia umeme,” alisema Mremi.

“Na vituo vingine vya jeshi likiwamo Duka la Jeshi lililoko JKT Oljoro na Njiro Nane Nane. Hii ni operesheni endelevu itakayowezesha shirika kujiendeshaā€¯.

Aidha Mremi alisema kufanyika kwa operesheni hiyo ni endelevu kwa ofisi hizo mkoa mzima, huku akisema Shirika hilo linalenga kukusanya madeni yote ya miaka iliyopita.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents