Habari

Tangazo la Nywele chanzo cha Maandamano Afrika Kusini

Waandamanaji nchini Afrika Kusini wamewalazimisha wenye maduka ya dawa na vipodozi kufunga maduka yao, baada ya kurushwa kwa tangazo la nywele ambalo wanadhani kuwa la ubaguzi wa rangi.

'Racist' shampoo advertisement sparks protests in South Africa

Tangazo hilo linaonesha picha za nywele za kiafrika zikiwa kavu na hazina muonekano mzuri wakati nywele za mtu mweupe zikionyeshwa kuwa nzuri na zinazovutia.

Chama cha upinzani cha ‘Economic Freedom Fighters (EFF)’ kimeliita tangazo hilo kuwa la kibaguzi na lisilojali utu.

Kiongozi wa chama hicho bwana Julius Malema ametaka maduka yanayouza bidhaa hiyo ya Clicks kufungwa.

Kampuni imetishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya chama hicho cha kisiasa lakini bwana Malema amewataka wafuasi wake kuwa tayari kwa mapambano na kusema EFF haiwezi kuogopa vitisho vyao.

EFF members outside the Clicks store in Goodwood Mall. On Monday morning, the EFF started their planned week-long occupation of Clicks stores, with members singing and dancing outside of multiple stores in Cape Town. Picture: Henk Kruger/African News Agency (ANA)

“Tangazo hili linamtambulisha mtu mweusi kuwa yuko chini ya mtu mweupe. Haya ni madai yanayotoa sifa za uzuri wa mtu mweupe kuwa ya kiwango cha juu na kuelezea jinsi rangi nyeusi inavyowakilisha ubovu, ubaya au jambo kutokuwa sawa,” taarifa ya EFF ilieleza.

Wanachama wa chama hicho, ambao huwa wanavalia mavazi ya rangi nyekundu ili kuonesha mshikamano na wafanyakazi, walifanya maandamano kama hayo mwaka 2018 dhidi ya nguo zinazotengenezwa na kampuni ya H&M baada ya kampuni kuchapisha jarida ambalo lilimuonesha kijana mweusi akiwa amevalia sweta lililoandikwa ‘nyani mzuri zaidi msituni’.

The SAHRC is conducting its own investigation into the Clicks advertisement debacle which has caused outrage.

Chama cha EFF, kilianzishwa mwaka 2013 na bwana Malema, na mara zote kimekuwa kikijitofautisha na chama tawala cha African National Congress (ANC) ambacho wanadai kimekuwa kikwazo katika wazo lake la mapinduzi.

Bwana Malema anadai kuwa ANC inawatenga maskini ambao wengi ni jamii ya watu weusi na badala yake wanawakilisha maslahi ya wafanyabiashara wakubwa ambao ni wazungu.

Clicks will be delisting and removing all TRESemmé products from shelf with immediate effect and will be replacing the gap with locally sourced haircare brands.

Wengi wanasema ubaguzi bado unabaki kuwa tatizo ambalo alijapatiwa ufumbuzi katika jamii ya raia wa Afrika Kusini, miaka 29 baada ya kumalizika kwa mapambano dhidi ya ubaguzi.

Tangazo hilo la Clicks lilitolewa mtandaoni wiki iliyopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents