Tanzania inatangazwa London

SERIKALI imesema, haikufanya kampeni ya matangazo ya utalii nchini Uingereza kwa sababu ya matatizo ya Kenya, bali ni mpango uliokuwapo kabla ya matatizo hayo ya kisiasa nchini humo.

Na Mwandishi Wa Mwananchi, London

 

 

 

SERIKALI imesema, haikufanya kampeni ya matangazo ya utalii nchini Uingereza kwa sababu ya matatizo ya Kenya, bali ni mpango uliokuwapo kabla ya matatizo hayo ya kisiasa nchini humo.

 

 

 

Akizungumza juzi katika uzinduzi wa kampeni ya matangazo ya Utalii jijini hapa nchini Uingereza, uliofanyika katika ubalozi wa Tanzania, Katibu Mkuu Wizara ya Malisili na Utalii, Blandina Nyoni alisema serikali iliweka bajeti yake ya matangazo tangu mwaka uliopita wa fedha na sasa kinachofanyika ni utekelezaji.

 

 

 

Nyoni alisema awali Serikali ilifanya kampeni hiyo nchini Marekani mwaka jana na kuzindua matangazo kwenye Televisheni ya CNN, hivyo awamu iliyobaki ilikuwa ni Ulaya na kuichagua Uingeleza kwani ndiyo inayoongoza kwa kuwa na watalii wengi.

 

 

 

Uzinduzi huo ulihudhuliwa na vyombo mbalimbali vya habari duniani, wafanyabishara, wawekezaji na wadau wa sekta ya utalii na kufuatiwa na kukatwa kwa utepe wa basi moja lililokuwa nje ya ubalozi wa Tanzania.

 

 

 

Tanzania imeamua kujitangaza na vivutio vyake ili kuhakikisha inapata watalii wengi zaidi na kuongeza pato la taifa .

 

 

 

� Tunaishukuru sana kampuni ya Jambo Publication kwa kutufanyia kazi hii, kweli imefanyika kama sisi tulivyofanya na tuna imani hata huko siku za baadaye tutaendelea kufanya nao kazi,� alisema Blandina.

 

 

 

Serikali inakusudia kuongeza matangazo zaidi ya utalii kwa Uingereza kwa sababu, imekuwa ikichangia sehemu kubwa ya pato la taifa kutokana na watalii wengi wanaongia nchini.

 

 

 

Tathmini ya watalii kutoka Uingereza inaonyesha kuwa, wanaotembelea Tanzania, mwaka 1997 walifikia 25,000 hadi 2006 walikuwa 69,160 na mwaka jana idadi yao iliongezeka.

 

 

 

Tanzania imeweka matangazo 100 kwenye mabasi yanayotoa huduma za usafiri katika Jiji la London na manne, Uwanja wa Ndege wa Heathrow. Matangazo hayo yameratibiwa na Jambo Publication chini ya Mkurugenzi wake, Juma Pinto.

 

 

 

Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents