Burudani

Tanzania ndio nchi pekee dunia ina muziki mgumu, Marekani hawahuwezi – AT

Msanii wa muziki Bongo, AT amedai kuwa Tanzania ina muziki wa pekee ambao ni vigumu kufanyika sehemu nyingine duniani na kuwataka wasanii kuona hiyo kama fursa.

AT amesema endapo wasanii watalijua hilo na kutengeneza muziki wenye utambulisho wa Kitanzania watapata nafasi zaidi ya wasanii kutoka Nigeria.

“Tunaweza kupata nafasi kubwa kuliko Nigeia, Tanzania ndio nchi pekee dunia ina muziki mgumu hawezi kutengenezwa Marekani, hiyo ni moja ya sifa ya nchi yetu, kwanini sasa tusizikamate hizi nafasi ambazo muziki wetu hata maprodyuza wakubwa hawezi kuufanya,” AT ameiambia Clouds TV.

AT ameendelea na kusema, “Tufanye kazi kwa ajili ya vizazi vinavyofuata, kufanya kazi kwa uadilifu na upendo, kufanya kazi yenye utambulisho wa Kitanzania pia itatupa sifa duniani,” .

November mwaka jana AT alishinda tuzo mbili katika ‘B&K Music & Video Music Awards’, vipengele alivyoshinda ni International Artist na Best Music Video kupitia wimbo wake ‘Sili Feel’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents