Habari

Tanzania yapokea Faru 9 kutoka Afrika Kusini

Usiku wa kuamkia leo Jumanne Septemba 10, 2019 Tanzania imepokea Faru 9 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakitokea Afrika Kusini.


Faru hao wameletwa na taasisi ya Grumet Fund na wamewasili saa 9 usiku kutoka katika hifadhi ya Thobatholo nchini Afrika Kusini.

Akizungumzia ujio wa Faru hao, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof Adolf Mkenda, amesema ujio wa Faru hao ni faraja katika uhifadhi na kuwataka Watanzania waendelee kuwalinda wanyama hao kwani ni mali ya Watanzania wote.

Prof. Mkenda akiongea na waandishi wa habari, amesisitiza kuwa uhai wa wanyamapori sio bora zaidi ya binadamu, Na hata lengo la kuwalinda ni kwa manufaa ya binadamu.

Hawa wanyama tunawalinda kwa manufaa ya binadamu, Kwahiyo binadamu ndio namba moja, wanyama wapo chini zaidi. Tunawalinda kwa sababu tunahitaji kipato cha kuendeleza nchi yetu, lakini tunajali zaidi uhai wa binadamu..  Na ndio maana mkurugenzi wa wanyamapori ameanza kuelezea hatua mbalimbali ambazo tunazichukua kwaajili  ya kuwalinda wananchi dhidi ya wanyamapori wakali na waharibifu,” amesema Prof. Mkenda.

Faru hao wenye asili ya Tanzania, watapelekwa katika eneo la Kiikolojia la Sasakwa Serengeti.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents