Habari

TANZIA: Mbunge wa Songea Mjini Mhe. Leonidas Gama afariki dunia

Mbunge wa Songea Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Leonidas Gama amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Peramiho, Songea.

Taarifa zinaeleza kuwa marehemu Gama alianguka nyumbani kwake saa saba usiku juzi huko Likuyu na kupooza upande wa kushoto akawa hajitambui kabisa ndipo alipopelekwa Hospitali ya Peramiho ambapo aliwekewa mashine za kumsaidia kupumua hadi umauti ulipomfika.

Gama amewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya na Ilala. Vilevile amewahi kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents