TANZIA: Salim Turky (Mr. White) mgombea Ubunge Zanzibar afariki dunia

Mwanasiasa mkongwe na mfanyabiashara maarufu Turk wa Zanzibar afariki dunia.

Mheshimiwa Salim Hassan Abdullah Turky, afariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa hospitali ya Tasakhta global chanzo cha kifo chake inadaiwa kuwa aliugua ghafla.

Swala ya maiti itafanyika leo Alasiri September 15 katika msikiti wa Othman Maalim na baada ya hapo atazikwa Fumba, Zanzibar.

Salim Turky alikuwa mfanyabiashara maarufu Zanzibar na mbunge wa jimbo la Mpendae tangu 2010, alizaliwa February 11, 1963. Mpaka anafariki alikuwa mwenyekiti wa makampuni ya Turky ambapo chini yake yalikuwa makampuni 12 yanayoendesha biashara zake Tanzania Bara, Zanzibar na visiwa vya Comoro.

Baadhi ya makampuni hayo yanajumuisha hoteli ya Golden Tulip, hospitali kubwa ya Tasakhtaa Zanzibar, pia ilijihusisha na biashara ya cement, Nitak communications, vyakula na mafuta.

Turks Group iliazishwa mwaka 1978 kama duka la nguo na ndugu wa familia moja ambao ni Salim, Murtadha na marehemu Yunus pamoja na baba yao, Hassan Turky na miaka 40 baadae wakalibadilisha kuwa moja ya makampuni yanayoongoza Tanzania.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW