Michezo

Tazama Goli bora la kujifunga kuwahi kutokea kwenye Soka

By  | 

Mchezaji wa klabu ya Pully Football inayoshiriki Ligi daraja la kwanza nchini Uswizi, Adrien Gulfo, amejifunga goli bora zaidi kuwahi tokea licha ya kuwa goli hilo limeiletea madhara timu yake ya Pully Football.

Katika mchezo huo, Gulfo, alikuwa akijaribu kuokoa mpira uliopigwa kwa kichwa na kuelekea langoni mwake, katika heka heka za kuokoa amejikuta akiupiga tikitaka katika na kuingia wavuni.

Sababu ya kua Goli bora zaidi la kujifunga ni kutokana na ugumu wa ‘Angle’ alioluwepo mpaka mpira ukatinga nyavuni.

Hata hivyo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya kufungana magoli 3 kwa 3 baada ya klabu ya Pully Football kutoka nyuma kwa goli moja na kisha mchezo huo kuamuliwa kwa mikwaju ya Penati , ambapo Pully Football ilichomoza na ushindi wa magoli 4 kwa 3 dhidi ya FC Renens.

BY HAMZA FUMO

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments