Tazama Picha jinsi Alikiba alivyoitikisa Tabora kwenye show yake ya jana usiku

Msanii Alikiba amefanya tamasha lake la Alikiba Unforgettable Tour, ambalo ni sehemu ya kuazimisha miaka yake 17 kwenye muziki, na ameanza Tabora usiku wa kuamkia leo Desemba 1, 2019 kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Alikiba akiwa jukwaani

Alikiba akiwa na wasanii wote wa Kings Music walipanda jukwaani na kuachia burudani kwa kuimba ngoma moja baada ya nyingine, ambapo Alikiba alipanda na Cinderella na kumaliza na ngoma yake mpya inayofanya vizuri kwa sasa ‘Mshumaa’.

Alikiba akitoa burudani

Baaada ya kupiga show kwa takribani masaa mawili alimkaribisha msanii Abdu Kiba, ambaye naye alipiga show kali kisha akawainua wasanii wa Kings Music Cheed, Killy na K2GA, ambao walipigiwa shangwe kubwa na wakazi wa Tabora waliofurika uwanjani.

Abdu Kiba alipopanda jukwaani

Baadaye Alikiba alirejea jukwaani tena akamtambulisha msanii mpya wa Kings Music Tommy Flavour, kisha akaweka wazi kuwa ngoma ya Tommy inayokuja humo ndani ameshirikishwa yeye.

Wasanii wa Kings Music wakiwa jukwaani

Alikiba Unforgettable Tour inapewa nguvu na East Africa Television na East Africa Radio, ambapo mbali na tamasha, Alikiba anafanya shughuli mbalimbali za kurejesha kwa jamii ikiwemo kutoa vifaa tiba pamoja na mahitaji kwa wagonjwa kwenye hospitali ya mkoa wa Tabora.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW