Tenga Apata Mpinzani Toka Mwanza

SIKU moja baada ya kutangazwa mchakato wa kutoa fomu za kuwania uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania, ambazo zinatolewa kwa Sh300,000 kwa rais na makamu wake, rais wa sasa, Leodegar Tenga amepata mpinzani jana.

SIKU moja baada ya kutangazwa mchakato wa kutoa fomu za kuwania uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania, ambazo zinatolewa kwa Sh300,000 kwa rais na makamu wake, rais wa sasa, Leodegar Tenga amepata mpinzani jana.

Hadi jana, mtu mmoja alikuwa amejitokeza naa kuchukua fomu ya kuwania urais wa TFF katika uchaguzi huo mwezi ujao.

Tenga alitangaza kuwania nafasi hiyo ya uongozi wa TFF katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Henry Tandau alitangaza kuanza kwa zoezi hilo lililoanza jana na tayari mkazi wa Mwanza, Richard Julius Lukambula amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania urais.

Mwakilishi wa mkazi huyo wa Mwanza ambaye hakutaka jina lake litajwe, alionyesha waandishi wa habari fomu hizo pamoja na risiti ya Sh300,000 ikiwa ni gharama za kuchukua fomu hizo.

Alisema kuwa ameagizwa na Lukambula ambaye ni Mjumbe wa Chama cha Soka Mwanza, MRFA kuchukua fomu hizo.

Kamati ya uchaguzi ya TFF ilitangaza juzi kuwa ndiyo siku ya kwanza kuchukua fomu kwa wagombea wa nafasi zote na mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu kuwa ni Novemba 14.

Akiainisha sifa za kugombea uongozi, Tandau alisema sifa ya rais, makamu wa kwanza na wa pili ni wenye shahada wakati katika nafasi nyingine wenye sifa ni kuanzia kidato cha nne.

Uchaguzi huo utakaogharimu Shilingi milioni 90 umepangwa kufanyika Desemba 14 kwenye Ukumbi wa NSSF Water Front jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo, wadau wa soka wamesema kuwa gharama hizo za kuchukulia fomu za kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi TFF zinastahili na zimezingatia hali ya uchumi.

Gharama za kuchukulia fomu zilizotangazwa na kamati hiyo ni katika nafasi ya rais, makamu wa kwanza na wa pili ni Sh 300,000, wakati katika nafasi za wajumbe wa TFF ni Sh200,000.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents