Tetesi: Inasemekana huyu ndiye mpenzi wa Diamond kutoka Rwanda (+picha/video)

Mara nyingi mastaa wengi hupenda kufanya mahusiano yao siri hadi pale habari zinapovuja ndipo wanaamua kuweka kila kitu wazi.

Mara baada ya kuachana na Zari The Boss Lady kumekuwa na tetesi kuwa Diamond anatoka na msichana maarufu hasa katika mitandao nchini Rwanda, Shaddy Boo.

Tetesi zinaibuka wakati kukiwa na stori kama hizo kuwa Diamond amerudiana na mwanamitindo Hamisa Mobetto ambao walifanya mahusiano yao kuwa siri hadi pale walipojaliwa kupata mtoto.

Taarifa zinaeleza kuwa Diamond na Shaddy wamekuwa karibu sana hasa muimbaji huyo anapokuwepo nchini Rwanda na kuna baadhi ya picha pamoja na video zinaeleza hilo.

Katika birthday ya Diamond October 02, 2017 iliyofanyika Hyatt Regency Dar es Salaam, Shaddy ni miongoni mwa watu waliyohalikwa.

Kama hiyo haitoshi katika show ya Diamond aliyofanya Naivasha, Kenya January 01, 2018 mrembo huyo alikuwepo na kuna baadhi ya picha zinawaosha wakiwa chumbani pamoja na Lukamba ambaye ni mpiga picha wa WCB.


Katika picha hizo mbili za mwanzo utaona Shaddy na Lukamba walikuwa hotel moja ukitazama kwa makini. Taa iliyo juu ya meza inaweza kuthibitisha hilo.

Picha ya juu ni kipindi ambacho bado Diamond alikuwa Kenya, utaona wawili hao kuna mmoja wapo wamevaa ‘sendo’ za mwenzake au wamevaa sare. Hata hivyo mwisho wa siku hizi zote zinabaki kuwa ni tetesi.

Pia inaelezwa kuwa Shaddy alikuwa ameolewa na producer Meddy Saleh kutoka Rwanda na walijaliwa kupata mtoto mmoja kabla ya kutengana.

Picha zaidi za Shaddy pamoja na video zake.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW