Habari

The Game amwaga $10,000 kwa waathirika wa kimbunga cha Sandy ili wakapige kura


Huenda Barack Obama ana haja ya kumpigia simu rapper The Game na kumshukuru kwa kuwasaidia wapiga kura 500 walioathirika na kimbunga cha Sandy kwenda kupiga kura. Inadaiwa kuwa The Game ametumia 10,000 kuwalipa wananchi hao wa New York waliokosa makazi baada ya kimbunga hicho ili waweze kwenda kushiriki zoezi hilo.

Game anasema hela hiyo ilikuwa ni kuwasaidia wananchi hao kununua mafuta ama njia nyingine ya usafiri ili kwenda kwenye vituo vya kupigia kura.

Hakuishia hapo bali pia alitumia gari lake kuwapeleka wengine kwenye vituo hivyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents