Michezo

Thierry Henry amtaja Paul Scholes kuwa ndiye mchezaji bora wa muda wote katika ligi kuu England

Mchezaji soka na gwiji wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, Thierry Henry amewafanya watu kubaki na mshangao kwa kumtaja kiungo wa zamani wa England na Manchester United, Paul Scholes kuwa ndiye mchezaji bora aliyewahi kukutana naye katika historia ya Premier League.

Scholes

Henry alijibu swali hilo katika interview moja na Sky Sport, alipotakiwa kumtaja mchezaji bora wa muda wote wa ligi kuu England.

Henry anasema Paul Scholes ndiye mchezaji pekee aliyeweza kuufanya mpira chochote na kwamba kwa mujibu wa Henry, Scholes amekuWa hapati heshima na sifa anazostahili.

“Paul Scholes ni bora zaidi mimi kuwahi kukutana naye. Timu ya taifa haikutambua ubora wake, lakini Manchester United waliutumia uwezo wake vizuri,” alisema.

Scholes-2

Henry amekuwa tofauti na mashabiki wengi ambao wamekua wakiwapa vipaumbele akina Shearer, Henry mwenyewe, Giggs na Cristiano Ronaldo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents