Burudani

T.I Kurudi Jela!

Mapema wiki iliyopita, msanii maarufu wa Hip Hop duniani Curtis Harris maarufu kama T.I alijikuta katiwa rumande pamoja na mke wake Tameka ‘Tiny’ Cottle kwa madai ya kupatikan na madawa ya kulevya.

Wawiili hao mbao wamefunga ndoa wiki chche zilizopita,walisimamishwa na Polisi maeneo ya West Hollywood wakiwa katika gari yao aina ya Maybach wakitoka kwenye party majira ya saa tisa asubuhi. T.I na mkeo waliachiwa baad ya kutoa dhamana ya dola elfu kumi kila mmoj.

Kukamatwa huku ni miezi mitano tu baada ya rapper huyo kutoka jela alipokuwa kwa muda wa miezi saba baada ya kukamatwa kwa kosa la kutaka kununua bunduki bila idhini ya Serikali.

T.I anaweza kujikuta anarudi magereza kwani kwa mujibu wa sheria huko Marekani, hakutakiwa kukutwa na makosa ya namna yeyote kwa muda wa miaka mitano.

Hadi sasa haijatambulika kama atarudi jela wala kwa muda gani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents