Michezo

Tiketi 1 kushuhudia pambano la Floyd Mayweather Vs Manny Pacquiao kuuzwa zaidi ya shilingi milioni 5.4!

Pambano kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao haliishi kuwa lililosubiriwa zaidi bali pia linatarajiwa kuwa pambano lenye thamani kubwa zaidi katika historia ya masumbwi duniani.

Floyd Mayweather Jr.
Floyd Mayweather atachukua asilimia 60 ya mapato yote kutoka kwenye pambano hilo

Hivyo hakuna ubishi kuwa kiingilio chake kitakuwa kikubwa kidogo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Forbes, tiketi moja ya kushuhudia pambano hilo inaweza kufika $3,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 5.4 za Tanzania.

Pambalo la mwisho lililoingiza fedha nyingi zaidi lilikuwa kati ya Mayweather na Canelo Alvarez jijini Las Vegas, September 14, 2013. Mwaka huo, bei ya kawaida ya tiketi ilikuwa ni $2,887.69.

Kwa namna ambavyo pambano kati ya Mayweather na Pacquiao limesubiriwa kwa hamu, bei ya kawaida ya tiketi zake inaweza kuwa hata zaidi ya $3,000.

“The MGM Grand is considered a small venue for such an enormous fight, which would make tickets even more expensive, on top of the high anticipation of the fight itself. It’s been a long time coming, too long in some eyes, but the public can rest assured that ticket prices won’t come cheap for The Fight of the Century when the two step in the ring for the first time,” wameandika Forbes.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents