Burudani

Tip Top Connection hatuko bize kama WCB – Dogo Janja

Msanii wa muziki Bongo, Dogo Janja amefunguka mchango wa Babu Tale ndani ya Tip Top Connection kwa sasa.

Hii ni baada ya Babu Tale kuwa sehemu ya menejimenti ndani ya lebo ya WCB na kuibua madai kuwa meneja huyo kaitelekeza Tip Top Connection.

Dogo Janja akiwa katika la Tamasha la Kuibua Vipaji vya Muziki mkoani Arusha amesema kuwa hilo halina ukweli wowote kwani wamekuwa wakishirikiana kwa mambo mengi.

“Hapana sio kweli, Babu Tale anasimamia kazi zangu sana sana ila kwamba huku Tip Top sisi hatuko bize kama Wasafi ndio maana unaoa muda wote yupo kule, hatuna matukio,” amesema.

“Lakini nikiachia wimbo utaona redioni nitaenda na Babu Tale, so mimi sina matukio mengi ndio maana kwenye kazi zangu anakuwa mara chache sana pale ninapomuhitaji,” ameeleza Dogo Janja.

Hata hivyo licha ya Dogo Janja kuwa Tip Top Connection anapata mchango mkubwa kutoka kwa Manzese Music Baby (MMB), menejimenti ambayo imeanzishwa na Madee.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents