Tip Top wachekelea tuzo

Tip Top wachekelea tuzo
TIP Top Organization inayosimamia kazi za wasanii mbalimbali wa muziki
wa kizazi kipya hapa nchini imefurahia kwa wasanii wake waliongia
kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo za muziki nchini kutwaa tuzo
hizo


Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Meneja wa Tip Top Connection, Babu Tale alisema kwamba, ushindi walioupata wasanii wake unawapa faraja ya kuwa wasanii wanaowasimamia wanajua wanachofanya.

Alisema anamshukuru Mungu kwa mafanikio hayo kwani karibu kila mwaka wasanii zaidi ya wawili wanaofanya kazi chini ya Tip Top Organization wamekuwa wakitwaa tuzo.

“Ni jambo la kumshukuru Mungu…kwa kuwa wasanii tunaowasimamia kazi zao kufanya vizuri, hali inayoonyesha kuwa wanajua nini wafanyalo na pia kuuchukulia muziki kama ajira,” alisema Tale.

Katika kinyang’anyiro hicho, familia ya Tip Top ilinyakua tuzo mbili kati ya nne walizoshindanishwa, ambako moja ilikuwa ya msanii bora wa kike iliyokwenda kwa Khadija Shaban ‘Keysha’ na ile ya wimbo bora wa reggae/Ragga iliyonyakuliwa na Tundaman na Spack kupitia wimbo wao wa ‘Nipe Ripoti’.

Mbali na wasanii hao, Tip Top pia inasimamia kazi za wasanii kama Z-Anto, Madee, Pingu, Deso, Nurdin na wengineo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents