BurudaniHabari

TMK Wanaume wasambaratika

TMK WanaumeKUNDI la muziki wa kizazi kipya la TMK Wanaume au Wanaume Family lenye maskani yake Temeke, Dar es Salaam limesambaratika. Kutokana na hali hiyo unaweza kuchagua neno la kutumia kuhusu hali ilivyo ndani ya kundi hilo.

TMK WanaumeKUNDI la muziki wa kizazi kipya la TMK Wanaume au Wanaume Family lenye maskani yake Temeke, Dar es Salaam limesambaratika.

Kutokana na hali hiyo unaweza kuchagua neno la kutumia kuhusu hali ilivyo ndani ya kundi hilo. Ama waweza kusema mambo yanakwenda segemnege, hobelahobela, hangahanga, msagunda, arijojo, shaghalabaghala au shelabela, yote yakimaanisha kwamba ni ovyoovyo, bila ya mpango maalumu au taratibu.

Habari zilizopatikana ndani ya kundi hilo na kuthibitishwa na Meneja wake, Said Fela na baadhi ya wasanii ni kuwa mambo sasa si shwari.

Kwa mujibu wa chanzo chetu ni kwamba mmoja wa waasisi wa kundi hilo, Juma Kassim ‘Sir Nature’ amejiengua kinyemela na wasanii wengine watatu.

“TMK Wanaume mambo hayapo vizuri, inasikitisha kuona wasanii wamegawanyika ikiwa ni miezi michache tangu kundi lisherehekee kutimiza miaka minne tangu lianzishwe.

“Lakini ndio maisha, Nature amejiondoa, lakini vichwa vingine bado vipo na vina nguvu ya kuendeleza makamuzi, watu wanasonga mbele, shujaa halilii bunduki,” kilisema chanzo chetu.

Source: Bongo5

{mos_sb_discuss:14}

Bongo5.com brings you the latest news from East Africa at your finger tips. If you have a story you’d like to share please send an email to [email protected]

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents