Michezo

TOKOMEZA RUSHWA: Shaffih Dauda na wagombea uongozi TFF wadakwa na TAKUKURU

Wadau mbalimbali wa soka wakiwemo wagombea wa uchaguzi katika nafasi mbalimbali za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wamekamatwa jijini Mwanza na TAKUKURU kwa kile kinachodaiwa wanasuka mbinu za kupitisha rushwa.

Baadhi ya waliokamatwa ni pamoja na Mtangazaji wa Clouds FM, Shaffih Dauda, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), Almas Kasongo, Elias Mwanjale, Leonald Malongo, Effam Majinge, Osuri Kasuli, Richard Kayenzi, Lazack Juma pamoja na Kelvin Shevi.

Tararifa kutoka kwa Msemaji Mkuu wa TAKUKURU, Ndg Ernest Makale amesema waliwakamata jana usiku jijini Mwanza kwa kuwekewa mitego sehemu wanazofanyia vikao vyao vya siri vya kusuka mianya ya rushwa kwa maandalizi ya kuelekea Uchaguzi mkuu wa Viongozi wa TFF utakaofanyika Agosti 12 mjini Dodoma.

“Tumewakamata kwa sababu hiki siyo kipindi cha kampeni na dalili zote kwamba walikuwa hapa kwa ajili ya uchaguzi unaotarajiwa zilikuwa zipo wazi, kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa tumeona kuna viashiria vya rushwa, tukaweka mitego katika sehemu walizokuwa wanaendesha vikao vyao vya siri tukaweza kuwakamata“,amesema Makale.

Hata hivyo, Ndg Makale amesema watuhumiwa hao wameachiwa kwa dhamana ila wanaendelea na uchunguzi wao endapo watakapopata ushahidi wa kutosha watafikishwa mahakamani.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents