Totoo Ze Bingwa azindua albamu
MWANAMUZIKI toka katika bendi ya Akudo Impact Totoo Ze Bingwa, amefanya utambulisho wa albamu yake mpya aambayo anatarajia kuingia sokoni julai 24 mwaka huu, baada ya jana katika uzinduzi huo kava la albamu hiyo kutokuwa tayari na kufanya isiuzwe papo kwa hapo.
Aidha alidai pia kama kuna mtu anahitaji kuuziwa albamu hiyo bila ya kava, basi angeuziwa.
Katika uzinduzi huo pia ulifanyika uzinduzi wa mwanamuziki mwingine toka Kenya Sharama, katika albamu yake ya Vunja Winga. ambayo yenyewe ilisambazwa na kuuzwa papo hapo kutokana na kukamilika kwa kila kitu.
Zaidi ya burudani, kulikuwa na sarakasi za hapa na pale
Fid Q naye alikuwa pamoja nao, kwa kuonyesha wapo pamoja.
Hili ni bonge la Koraborasheni la Zola D, Abas na Shara aliyevaa kofia.
Benjamini wa Mambojambo naye alikuwepo hapo katika kuhakikisha burudani ikifikia kwenye kiwango chake.
Christian Bella naye alikuwa sambamba na Akudo kwaajili ya kumsindikiza mwanamuziki mwenzao.