Habari

Trailer: Rapper Ja Rule kuja na filamu mpya ‘I’m In Love With A Church Girl’

Baada ya kumaliza kifungo chake na kutoka jela mwezi May mwaka huu, rapper mkongwe Jeff Atkins maarufu kama Ja Rule kuja na movie mpya.

ja-rule1

Katika filamu hiyo inayoitwa ‘I’m In Love With A Church Girl’, Ja Rule (37) ambaye ameigiza kama Miles Montego, amecheza kama mtu mwenye maisha flani ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, wanawake, matumizi makubwa ya pesa, magari nk. Mpaka alipokuja kukutana msichana wa ndoto zake, binti mzuri na mcha Mungu aitwaye Vanessa ambaye Ja Rule ‘Montego’ alimzimia.

Wahusika katika filamu hiyo ni pamoja na Jeff “Ja Rule” Atkins , Adrienne Bailon, Stephen Baldwin, na Michael Madsen.

Hii itakuwa si fimalu ya kwanza kwa raaper huyu wa Murder Inc kucheza, Ja Rule amewahi kuigiza katika ‘The Fast and the Furious’ ya (2001), ‘Scary Movie 3’ ya (2003) na ‘The Cookout’ ya (2004).

‘I’m In Love With A Church Girl’ inatarajiwa kuachiwa rasmi Marekani October 18 mwaka huu.

Tazama Trailer ya movie hiyo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents