Burudani

Twanga kuinadi Dunia daraja Chalize

new_years_eve_048

Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” ijumaa hii tarehe 06-01-2012 inataraji kufanya onyesho mahsusi kwa ajili ya kuinadiĀ  albamu yake mpya iliyo sokoni hivi sasa ya Dunia Daraja katika ukumbi wa Ndelema Inn uliopo Chalinze mkoa wa Pwani.

Twanga Pepeta ambayo katika historia yake ilishawahi kufanya onyesho moja tu katika wilaya hiyo, itatumia onyesho hilo kwa ajili ya kuwapa wapenzi wa muziki wa Dansi wa Chalinze zawadi ya mwaka mpya wa 2012 kwa kuwapa burudani safi kupitia kikosi cha wanamuziki wake mahiri wakiongozwa na Kiongozi wao Luizer Mbutu.
Kupitia onyesho hili, Twanga Pepeta inataraji kuuza CD zenye kazi zao zote kuanzia Kisa Cha Mpemba albamu ya kwanza mpaka Dunia Daraja albamu ya 11. Nyimbo zinazopatikana kwenye albamu ya Dunia Daraja ni pamoja na Mapenzi Hayana Kiapo, Kauli, Mtoto wa Mwisho, Dunia Daraja, Umenivika Umasikini na Penzi la shemeji.
Mara baada ya onyesho kumalizika Twanga Pepeta itaendelea na ratiba yake ya maonyesho kama kawaida kwa kesho yake kufanya onyesho katika ngome yake ya Mango Garden na Jumapili itamalizia kufanya onyesho katika viwanja vya Leaders mchana na usiku watamalizia kutoa burudani T.C.C Chang’ombe.new_years_eve_059
Picha za mwaka mpya, Hadija Kimobitel na Densa.
new_years_eve_046

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents