Burudani ya Michezo Live

Ufaransa yamtangaza Waziri Mkuu mpya

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amemteua Jean Castex kuwa Waziri Mkuu mpya, kama sehemu ya kuifanyia mabadiliko serikali yake.

Macron names senior official Jean Castex new French PM | Daily Sabah

Ikulu ya Ufaransa, Elysee imesema leo kuwa Castex, mwenye umri wa miaka 55, amekuwa akiongoza mkakati wa Ufaransa wa kupunguza hatua za kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona. Macron amemuagiza Castex kuunda serikali.

Uteuzi wa Castex, ambaye ni mtumishi wa umma umefanyika saa chache baada ya Edouard Philippe pamoja na serikali yake yote kutangaza kujiuzulu mapema leo.

France's Macron picks Jean Castex as PM after Philippe resigns ...

Macron anafanya mabadiliko ya serikali ili kuangazia zaidi katika kuufufua uchumi wa nchi hiyo baada ya miezi kadhaa ya kuwepo kwa vizuizi vilivyowekwa ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona. Baraza la mawaziri la Ufaransa linatarajiwa kutangazwa ifikapo Jumatano ijayo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW