Michezo

Ufisadi TFF: Ndoto ya Malinzi kutetea kiti chake yayeyuka ghafla

Rais wa Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ambaye anakabiliwa na tuhuma za utakatishaji fedha na kughushi nyaraka za Shirikisho hilo ili ajipatie fedha huenda tusimuone tena kwenye kinyang’anyiro cha kugombea Urais kwani tayari ameswekwa rumande kwa mpaka Julai 3 ya mwezi mwaka huu.

Rais Jamal Malinzi akiwa katikati na Makamu wake Celestine Mwesigwa.

Malinzi hataweza kutetea kiti chake kwani zoezi la usaili kwa wanaogombea nafasi mbalimbali za uongozi (TFF) limeanza leo mpaka Jumamosi ya tarehe 1 Julai na yeye kawekwa rumande mpaka jumatatu ya tarehe Julai 3.

Malinzi amefikishwa leo mahakamani akiwa na katibu wake, Mwesigwa Celestine wakikabiliwa na mashitaka 28, katika mashitaka hayo Jamal Malinzi anakabiliwa na mashitaka zaidi ya 25 mengi yakiwa ni ya kughushi nyaraka zaidi ya 20 za malipo katika michakato ya malipo mbalimbali .

Shitaka lingine ni la utakatishaji fedha na hii ni kwa wote watatu, Malinzi, Mwesigwa na na Afisa wa fedha wa TFF, Nsiande Mwanga wanatuhumiwa kutakatisha kiasi cha zaidi ya dola laki 3 za kimarekani.

Viongozi wenza wa ugombea nafasi ya Urais TFF ni Ally Mayay, Jamal Malinzi, Frederick Mwakalebela na Wallace Karia.

Je, wewe kama mdau wa soka ni kiongozi gani unaona atalipeleka soka letu mbele kati ya hao waliobaki kwenye nafasi ya Urais?

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents