Habari

Ugonjwa usiojulikana waibuka China, virusi vyake vyaenea kwa kasi

Sampuli ya virusi vya ugonjwa vilivyochukuliwa kutoka kwa mgonjwa na kuchunguzwa katika maabara na maafisa wa serikali pamoja na wale wa shirika la afya duniani WHO zimethibitisha kwamba ugonjwa huo ni ule wa Coronavirus.

Image result for China coronavirus

Virusi hivyo ni familia kubwa ya virusi sita na kirusi hicho kipya kitaongeza idadi hiyo kufikia saba ambapo ni maarufu kwa kusababisha maambukizi miongoni mwa binadamu.

Virusi hivyo vinaweza kusababisha homa, lakini pia vinaweza kusababisha ugonjwa mbaya wa Sars ambao uliwauwa watu 774 kati ya 8,098 walioambukizwa katika mlipuko ulioanza China 2002.

Uchanganuzi wa jeni za ugonjwa huo mpya unaonyesha kuhusishwa karibu na ugonjwa wa Sars zaidi ya ugonjwa wowote wa Coronovirus.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Mamlaka ya China imeripoti visa 139 vipya vya ugonjwa huo usiojulikana katika siku mbili, ikiwa ni mara ya kwanza kwa maambukizi hayo kuthibitishwa nchini humo nje ya mji wa Wuhan.

Visa vipya vya viruzi hivyo vilibainika katika miji ya Wuhan, Beijing na Shenzhen. Korea Kusini pia iliripoti kisa chake cha kwanza kilichothibitishwa siku ya Jumatatu baada ya Thaialnd na Japan.

Jumla ya visa vilivyoripotiwa sasa vinapita 200 na watu watatu tayari wamefariki kutokana na virusi hivyo.

Image result for China coronavirus

Maafisa wa Afya wamegundua ugonjwa huo, ambao kwa mara ya kwanza ulipatikana mjini Wuhan mwezi Disemba.

Wanasema umesababisha mlipuko wa homa ya mapafu lakini mengi kuuhusu haujulikani.

Wataalama nchini Uingereza waliambia BBC kwamba idadi ya watu walioambukizwa huenda ikawa kubwa zaidi ikilinganishwa na idadi iliotolewa na maafisa huku takwimu zikisema huenda imefikia watu 1,700.

China imeahidi kuongeza juhudi zake za kuchunguza wiki hii ya sherehe za kuadhimisha mwezi mpya ambapo mamilioni ya Wachina watasafiri kujiunga na familia zao.

Je ni nani aliyeambukizwa?

Mamlaka katika mji wa kati wa Wuhan nchini China inasema kwamba visa vipya 136 vimethibitishwa wikendi iliopita na mtu watatu katika mji huo akafariki kutokana na virusi hivyo.

Kwa jumla mji huo pekee umethibitisha karibia visa 200 vya ugonjwa wa Coronavirus.

Kufikia Jumapili jioni , maafisa wanasema kwamba takriban watu 170 mjini Wuhan walikuwa wanatibiwa hospitalini , ikiwemo watu tisa ambao walikuwa katika halli mahututi.

Maafisa wa afya katika wilaya ya Daxing mjini Beijing, walisema kwamba watu wawili waliosafiri kuelekea Wuhan walitibiwa ugonjwa wa homa ya mapafu unaohusisswa na virusi hivyo.

Mjini Shenzhen , maafisa walisema kwamba mtu mwenye umri wa miaka 66 alionyesha ishara ya virusi hivyo baada ya kuitembelea jamii yake huko Wuhan.

Virusi hivyo pia vimesambaa ugenini. Visa viwili vilithibitishwa nchini Thailand kimoja Japan – vyote vikuhusisha watu kutoka Wuhan ama wale waliotembelea mji huo.

Korea Kusini iliripoti kisa chake cha kwanza kilichothibitishwa kuhusu ugonjwa huo siku ya Jumatatu.

Kituo cha udhibiti wa magonjwa ya mapafu nchini Korea kilisema kwamba mwanamke mmoja wa China mwenye umri wa miaka 35 alikuwa akiugua mwili kuwa na joto na tatizo la kupumua alipowasili nchini humo baada ya kutoka Wuhan.

Alitengwa na kutibiwa katika hospitali moja , walisema.

Maafisa wanasemaje?

Tume ya kitaifa ya afya nchini China siku ya Jumapili ilisema kwamba virusi hivyo vinaweza kukingwa na kudhibitiwa , huku akionya kwamba uchunguzi wa karibu unahitajika kwa kuwa chanzo cha maambukizi hakijulikani.

Wamesema kwamba hakukuwepo na visa vya virusi hivyo kusambaa kutoka mtu mmoja hadi mwingine lakini na kwamba vimevuka mpaka na kuingilia spishi kutoka kwa wanyama walioambukizwa baharini na soko la wanyama mwitu katika mji wa Wuhan.

Shirika la Afya duniani linasema kwamba vyanzo vya wanyama vinadaiwa kuwa chanzo kikuu cha virusi hivyo na kwamba kulikuwa na visa vichache vya maambukizi ya binadamu hadi binadamu wanaposhikana.

”Huku visa vingi vikifichuliwa na uchanganuzi zaidi ukifanywa, tutapata picha nzuri kuhusu athari ya ugonjwa huo na maeneo ulioambukizwa”.

Ilisema kwamba ongezeko la idadi ya visa hivyo nchini China linatokana na kuongezeka kwa mipango ya vipimo na utafiti wa virusi hivyo miongoni mwa wagonjwa wanaougua magonjwa ya mapafu.

”Watu wanaweza kupunguza hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo kwa kuchukua hatua kama vile kuzuia kushikana na wanyama, kupika vizuri nyama na mayai na kuzuia kushikana na mtu yeyote mwenye ishara za homa”, ilisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents