Habari

Uingereza yatoa msaada kusaidia watu wenye matatizo ya macho mkoani Singida

Shirika lisilo la kiserikali la Sight Savers la Uingereza, limetoa msaada wa zaidi ya Sh2.2 bilioni kugharamia Mradi wa Maono Singida unaotarajiwa kutekeleza kwa miaka minne.

macho

Fedha hizo zimetolewa kupitia Benki ya Standard Chartered ya nchini humo kama msaada ili kutekeleza mpango wake wa ‘kuona ni kuamini’.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Taifa wa Huduma za Macho nchini, Dk Nkundwe Mwakyusa wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Kanisa la Katoliki mjini hapa.
Alisema wilaya zitakazonufaika na mradi huo ni Ikungi, Manyoni, Mkalama na Singida.

Dk Mwakyusa alisema mradi huo utahusisha kujenga miundombinu mbalimbali, kuimarisha huduma za macho na kutoa mafunzo kwa wataalamu. Pia, alisema yapo madhara mengi yatokanayo na matatizo ya macho ikiwamo wajukuu wa wazee wenye upofu kutumia muda mwingi kuwahudumia badala ya kuhudhuria masomo shuleni.

Awali, Mganga Mkuu wa mkoa huo, Dk John Mwombeki alisema kuna wataalamu wachache wa huduma ya macho na vitendea kazi duni.

“Kwa hiyo ujio wa mradi huu utapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto zinazotukabili,” alisema.
Alisema madhara yatokanayo na upofu huathiri jamii nzima.

Shirika la Sightsavers lilianzishwa mwaka 1950 kwa lengo la kupambana na upofu duniani. Kwa Tanzania lilianzishwa mwanzoni mwa miaka ya 1970 na hivi sasa liko kwenye mikoa 17.

Source: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents