Habari

Ulaya yataka suluhisho mgogoro Iran na Marekani, Rais Hassan Rouhani asema taifa hilo limefeli

Mawaziri wa mambo ya nje wa Ulaya, wanakutana hii leo mjini Brussels,  kujadili namna ya kuzishawishi Iran na Marekani kupunguza mvutano na kukaa katika meza ya mazungumzo.

Japan Osaka | G20 Gipfel | Emmanuel und Angela Merkel (Reuters/J. Silva)

Mgogoro kati ya Iran na Marekani umezidi kufukuta tangu Raisi wa Marekani Donald Trump alipoamua kujiondoa katika makubaliano hayo ambapo Iran ilikubali kupunguza shughuli za uundaji wa silaha za nyuklia, kwa sharti la kupunguziwa vikwazo vya kiuchumi na Marekani.

Kutokana na Marekani kuiwekea tena vikwazo vikali, ambavyo vinaulenga moja kwa moja mfumo wa mapato wa nchi hiyo unaotokana na mafuta, Iran imeendeleza majukumu yake ya uzalishaji wa silaha za nyuklia kukiwa bado na makubaliano.

Rouhani asema Marekani imefeli

Kwa mujibu wa shirika la habari la DW, Akizungumzia mgogoro kati ya nchi yake na Marekani katika moja ya hotuba zake, Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema kuwa kila jaribio ambalo Marekani imelifanya dhidi ya Iran ndani ya miezi hii 14, liwe kwa njia za kijamii, kisiasa ama kisheria limefeli halikufanikiwa.

Katika Umoja wa Mataifa kwenye mikutano mbalimbali, na uwepo wao wiki iliyopita kwenye Shirika la kimataifa la nishati na Atomiki, ambalo lilionesha kuwa hakuna hata nchi moja duniani ambayo ingesikiliza tuhuma zao.  Kando ya Marekani na baadhi ya nchi, mataifa mengine yote yaliilinda Iran.

Iran Teheran - Hassan Rouhani hält Ansprache zum Army Day (Getty Images/AFP)Rais wa Iran Hassan Rouhani

Kutokana na msuguano huo, nchi zenye nguvu za Ulaya, Ufaransa Uingereza na Ujerumani, zimeionya Iran kuwa imeshindwa kuzingatia masharti ya makubaliano hayo.

Mataifa hayo matatu, ambayo ni washirika katika makubaliano hayo  sambamba na Urusi, na China, yanatafuta namna ya kututatua mgogoro huo ambao umesababisha Marekani kuanzisha mpango unaolenga mashamblizi ya anga dhidi ya Iran, ambao Rais Trump aliusitisha katika dakika za mwisho.

Raisi wa Ufaransa Emmanuel Macron, alimtuma mwanadiplomasia wake wa juu kwenda Iran wiki iliyopita ili kupendekeza namna ya kuituliza hali na kwamba alitaka kupitia upya maendeleo ya kidiplomasia ifikapo leo Julai 15.

Siku ya Jumapili, Raisi Rouhani Rouhani alisisitiiza msimamo wake kuwa Iran iko tayari kufanya majadiliano na Marekani, iwapo Marekani itaviondoa vikwazo ilivyovirejesha kwa Iran kuhusiana na mpango wa nyuklia.

Hata hivyo Trump, hajaonesha dalili yoyote ya ya kuondoa vikwazo hivyo licha ya kujadili na Raisi wa Ufaransa  na alisema wiki iliyopita kuwa ataongeza vikwazo zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents