Burudani

Umeme waota mbawa

1

Haya sasa huu ni wakati wa kujikumbusha ule wimbo wetu, kila kitu kimepanda bei hasa baada ya kutangazwa bei mpya ya nishati ya umeme na  Mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji (Ewura).

Ingawa wanasiasa bado wamesimama katika upande ambao wanaiomba shirika hilo lenye mamlaka makubwa ya kufanya uchumi wan chi kupanda au kushuka kutoka wao kuwa kama nguzo ya  maendeleo ya nchi, kwa kuzalisha nishati ambayo inatumiwa na kila mtu, kwamba wakusanye   marimbikizo ya madeni yanayokaribia sh bilioni 300 toka kwa wadaiwa, kuliko mzigo huo kuwaongezea wananchi.

Wanasema wananchi ambao wanatumia umeme wa Unit 50 kwa mwezi wao mkumbo huo hautawagusa kwakuwa wao ni walala hoi. Hapo ndipo inakubidi urudi kwenye mita yako na kuchukua peni na karatasi, kisha unagawa hamsini kwa siku tharasini, hiyo namba utakayo ipata ndiyo itakupasa utumie kwa siku kama utaweza.

Kama hauwezi bassi ujue umeingia kwenye mkumbo wa ongezeko la asilimia 40.29, na utaiilipa ingawa wachunguzi wa mambo ya uchumi wanasema kwa sasa Maisha yamepanda kwa asilimia 20, na ukijumlisha na umeme utapata jibu la maisha yako harisi.

Aidha baadhi ya watu wanuliza kwa kusema kwamba, kama tatizo la umeme ni maji kwanini wasitumie umeme wa Songas, Simbion Power na TPTL, kwakuwa rais aliongea kwa alisema kwamba lazima nchi iwe na umeme wa uhakika na wabei nafuuuuuuuu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents