Habari

Upendo Mara tu Umuonapo?

Tumezoea kukisikia katika nyimbo, na kukiona katika filamu, na kukisoma vitabuni kioja hiki kiitwacho upendo. Lakini kweli mtu anaweza kupenda ghafla tu bila hata kumfahu mtu? Huo ni upendo wa kweli?
Mtu mwenye hisia za kimapenzi atasema ndio bila wasiwasi, lakini yule aliyekwisha yaona mambo au mhalisia atasema kuwa haiwezekani katu kumpenda mtu mara umuonapo kufuatana jinsi tunavyofafanua neno upendo.

Maelezo maarufu ya upendo hupatikana katika Wakorinto 12 Agano Jipya la Biblia, ambapo Paulo mwandishi wa kitabu hiki huanza kwa kusema, “Upendo ni uvumilivu, upendo ni mwema.” Sura hii huendelea vizuri sana ikieleza sifa nyingi za upendo.

Kwa maana hiyo upendo ni chaguo, siyo hisia. Sisi tunaamua kumpenda fulani, ndio maana suala zima la kumpenda mtu bila hiari yako inaleta wasiwasi, kwa sababu upendo ukichukuliwa kama hisia, hapo ndipo matatizo hujitokeza.

Ni kweli unaweza kuwa na hisia kwa ajili ya mtu fulani, lakini hebu tuseme wewe umemkasirikia mtu huyo,  ambaye unadai unampendsa utasema humpendi tena kwa sababu sasa umepata hisia za hasira? Hisia zina tabia ya kuja na kuondoka!

Huko India, na nchi nyingine wana desturi za kupanga ndoa. Huenda suala hili likaonekana kuwa la kizamani kwa wengi wenu, lakini takwimu zaonesha kuwa wale wanaofunga ndoa za  kupangiwa kulingana na wale walofunga ndoa za “mapenzi”, wale wa kwanza ndoa zao zinaendelea na kiwango cha talaka ni kidogo sana.

Wataalamu husema kuwa hii hutokea kwa sababu wale wafungao ndoa za mapenzi huweka kila kitu juu ya misingi ya kihisia na hisia zikipotea au wasipozipata hisia hizo tena, ndoa huvunjika.lakini wale ambao hufunga ndoa za kupangiwa, iliwabidi kwanza wajifunze kuthaminiana na hatimaye kuamua wa kupendana.

Hapa Tanzania, tunaona jinsi talaka zinavyoongezeka kwa kasi, na msururu wa mahusiano yaliyovunjika.tunaweza kuwa na nadharia nyingi kuhusu sababu za kueleza suala hili, lakini hatimaye ufikamo kwenye chanzo tunaweza kusema kwa ukweli kuwa wengi wetu tumechukua mwelekeo wa kiakili wa wanaashki. Kila kitu tumekiweka juu ya hisia. Tunataka cheche, ashki, kimia, lakini kihalisi mambo hayo hayatakuwepo kila mara. Ndipo hapo maisha ya kweli yanapoanza.

Jambo la kuzingatia ni kwamba, ndoa nyingi zenye kufanikiwa, zimeweza kufanya hivyo kwa sababu wanandoa hao hapo mwanzo walikuwa marafiki. Jambo lingine linalozingatiwa ni kwamba katika ndoa zenye mafanikio wanandoa hao wawili hawana zile sifa zote ambazo kila mwenzi anatarajia kupata kutoka kwa mwenziwe, jambo ambalo linatuonesha kuwa ni bora kuacha kuandika orodha za sifa tunazozipenda katika patna wetu na tuwe wawazi zaidi kwa uwezekano wa kwamba kile tunachokitaka huenda siyo kinachotufaa maishani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents