Habari

‘Upendo na Star Times’ yazinduliwa

startimes
Kampuni ya Starmedia imezindua promosheni ijulikanayo kama ‘Onyesha upendo na Startimes’, iliyolenga kuwanufaisha watumiaji wa king’amuzi na wateja wapya kujishindia zawadi mbalimbali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo jana, Makamu wa rais wa Starmedia, Bella  Xiong alisema mbali na zawadi ambazo kampuni hiyo imeona itoe  kwa wateja wake katika msimu huu wa sikukuu ya wapendanao, pia wamekusudia kushiriki katika matembezi maalum na kula chakula na watoto yatima katika moja ya kituo kama sehemu ya upendo wao katika kipindi hiki.

Kuhusu promosheni hiyo, Xiong alisema Starmedia imekusudia kutoa zawadi ya Televisheni moja kubwa, ving’amuzi  kumi pamoja na vocha 100 za ving’amuzi hivyo na kwamba mchakato mzima wa promosheni hiyo utafanyika kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuanzia sasa.

Kwa upande wake, Ofisa masoko wa starmedia Davis Mwijage, alisema kampuni hiyo mbali na kuamua kuonyesha upendo huo kwa kuendesha promosheni hiyo kwa watumiaji wa king’amuzi hicho, pia wamelenga kuongeza ufanisi kwa kuendelea kutoa huduma bora.

Alisema katika kutoa huduma hizo wamekusudia kuongeza mtandao wake katika mikoa ya Mbeya na Arusha na kwamba lengo ni kuifikia mikoa yote ifikapo mwishoni mwa mwakani.

Aidha Mwijage aliwataka watanzania kuendelea kujiunga na mfumo huo mpya wa digitali ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents