Michezo

USAJILI: Tetesi za usajili barani Ulaya

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania, Robert Fernandez amesema itakuwa “vigumu” kumsajili kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho mwenye umri wa miaka 25, kwa sababu hana kipengele cha uhamisho kwenye mkataba wake. (Liverpool Echo)

Barcelona “watapigana” mpaka siku ya mwisho ya usajili ili kumsajili Philippe Coutinho kutoka Liverpool. (Telegraph)

Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea ya Uingereza, Diego Costa mwenye umri wa miaka 28, amesema hatorudi Stamford Bridge na bado msimamo wake upo pale pale wa kujiunga na Atletico Madrid. (Telegraph)

Tokeo la picha la Diego Costa

Everton huenda wakamsajili, Diego Costa kwa mkopo. (Sun)

Beki wa Tottenham, Kevin Wimmer mwenye umri wa miaka 24, anazungumza na Stoke City kuhusu uhamisho wake wa pauni milioni 15. (Telegraph)

Stoke City pia wanataka kumsajili Kevin Wimmer kutoka Spurs. (Stoke Sentinel)

Beki wa Arsenal Gabriel, 26, anakaribia kujiunga na Valencia kwa pauni milioni 10. (Evening Standard)

Paris Saint-Germain bado wanataka kumsajili kiungo mkabaji wa Monaco, Fabinho, 23. (L’Equipe)

Manchester United wanataka kumsajili kiungo wa Monaco Thomas Lemar. (Daily Record)

Manchester United bado wana matumaini ya kukamilisha usajili wa Ivan Perisic. (Mirror)

Tottenham wamefikia makubaliano ya kimsingi ya kumsajili Davinson Sanchez, 21, kutoka Ajax kwa pauni milioni 28 na milioni 14 zaidi kama marupurupu. (Independent)

Manchester City wapo tayari kuwapa West Brom pauni milioni 22 ili kumsajili nahodha wao Jonny Evans, 29, baada ya dau la pauni milioni 18 kukataliwa, na watampa mara mbili ya mshahara wa pauni 75,000 kwa wiki anaolipwa sasa. (Mirror)

Dau la Chelsea la pauni milioni 62 kumtaka beki wa Juventus, Alex Sandro limekataliwa. (Mirror)

Tokeo la picha la Juventus, Alex Sandro

Chelsea wanajiandaa kumuuza Diego Costa kwa hasara. (Sun)

Kiungo wa PSG, Blaise Matuidi 30, amekamilisha vipimo vya afya Juventus, lakini timu hizo mbili bado hazijakubaliana jinsi ada ya uhamisho itakavyolipwa, huku meneja wa PSG, Unai Emery akisema hakutaka kumuuza mchezaji huyo. (Le Parisien)

Wakurugenzi wa Borussia Dortmund wamesema Barcelona “hata hawapo karibu” katika kufikia dau la mshambuliaji wake Ousmane Dembele, 20. (Kicker)

Fiorentina wamemwambia mshambuliaji wake Nikola Kalinic, 29, anayenyatiwa na AC Milan kuwa atapigwa faini kwa kutotokea mazoezini siku ya Alhamisi. (Sun)

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents