Michezo

USAJILI: Tetesi za usajili barani Ulaya  

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema lazima auze wachezaji kwanza kabla ya kununua wengine kwa sababu timu hiyo ina “wachezaji wengi mno”. (Independent)

Tokeo la picha la WENGER

Mkurugenzi mkuu wa Borussia Dortmund, Hans-Joachim Watzke ameituhumu Barcelona kwa kutokuwa na utaratibu mzuri katika kutaka kumsajili, Ousmane Dembele. (Daily Mail)

Wachezaji wa Leicester wamemwambia, Riyad Mahrez mwenye umri wa miaka 26, anayetaka kuondoka, abakie na klabu hiyo. (Leicester Mercury)

Tokeo la picha la Riyad Mahrez

 West Ham wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Sporting Lisbon, William Carvalho mwenye umri wa miaka 25. (Sky Sports)

Antalyaspor ya Uturuki imempa, Samir Nasri mkataba wa miaka miwili na mshahara wa pauni 70,000 kwa wiki ili kumsajili kutoka Manchester City. (Times)

Meneja wa Crystal Palace, Frank de Boer amesema bei ya beki wa Liverpool Mamadou Sakho, 27, ni kubwa mno. (Guardian)

Manchester United wanatarajia, Zlatan Ibrahimovic atasaini mkataba mpya wa kubakia Old Trafford wiki hii. (ESPN FC)

Manchester City wapo tayari kuvunja rekodi ya dunia kwa kutoa pauni milioni 275 na kutengua kipengele cha ada ya uhamisho cha Lionel Messi wa Barcelona. (Yahoo Sport)

Maafisa wa Manchester City wamekutana na wawakilisji wa Lionel Messi, 30, kujadili uwezekano wa mshambuliaji huyo wa Barcelona kuhamia Etihad. (Daily Record)

Lionel Messi alijiunga na Barca akiwa na miaka 13

Arsenal wamempa Alex Oxlade Chamberlain, 24, mkataba wa miaka minne na mshahara wa pauni 125,000 kwa wiki ili kuzuia Chelsea kumchukua. (Daily Star)

Nahodha wa Barcelona Andres Iniesta, 33, ambaye mkataba wake unaisha mwakani amesema hana uhakika wa kubakia na timu hiyo. (El Pais)

Barcelona wapo tayari kulipa pauni milioni 36 ili kumsajili kiungo wa Nice Jean, Michael Seri mwenye umri wa miaka 26, wakiwa na matumaini kuwa atacheza na Philippe Coutinho msimu ujao. (Mundo Deportivo)

Chelsea na AC Milan wanafuatilia mwenendo wa Pierre Emerick-Aubameyang, baada ya mshambuliaji huyo wa Borussia Dortmund kusema anahitaji kuondoka ili aweze kukua kisoka. (Radio Montecarlo Italy)

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents