Michezo

USAJILI: Tetesi za usajili barani Ulaya

Tetesi za usajili barani ulaya klabu ya Bournemouth wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza Jermain Defoe, kwa uhamisho huru kutoka Sunderland.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza, Jermain Defoe

Defoe,34 amerejea katika dimba la Vitality kwa mkataba wa miaka mitatu ambapo pia aliwahi kukipiga katika klabu hiyo mwanzoni mwa maisha yake ya soka.

Lyon wamekamilisha usajili wa beki kutoka Le Havre, Ferland Mendy kwa mkataba wa miaka mitano.

Aliyekuwa beki wa klabu ya Le Havre, Ferland Mendy (katikati)

Taarifa kutoka Sky Sports zinasema kwamba Crystal Palace, West Brom, Brighton na Birmingham walikuwa wanamuhitaji beki huyo mwenye umri wa miaka 22.

Hata hivyo Lyon wameshinda mbio hizo za kumnasa beki huyo na kumpa mkataba mpaka mwaka 2022.

Straika wa Arsenal Alexis Sanchez amesema kwamba ameshaamua wapi atacheza msimu ujao. Lakini nyota huyo wa Chile hakuthibitisha kwamba atakuwa timu moja na Golikipa wa Chile , Claudio Bravo pale Manchester City au atabaki na Gunners.

Mchezaji wa timu ya taifa ya Chile na klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez

Sanchez, ambaye mkataba wake unafikia kikomo majira yajayo ya kiangazi kwa sasa yupo kwenye majuku ya timu ya taifa ambapo kocha wake Juan Antonio Pizzi amemuelezea Sanchez kwamba ni mchezaji ambaye kila timu inamuhitaji.

Alipoulizwa kwamba ataungana na Bravo katika klabu ya City, Sanchez alisema,” Swali zuri. Sasa hivi akili yangu ipo kwenye mashindano ya kombe la Mabara. Pindi yatakapoisha ndio nitajua kwamba naondoka au nabaki. Sijui.”

Sanchez alipoulizwa kwamba anajua akilini kwake wapi atacheza msimu ujao, alisema,” ndio najua wazi kabisa, lakini siwezi kukuambia.”

Na kuhusu anatoa nafasi kiasi gani kwa yeye kubaki Arsenal msimu ujao, Sanchez alisema,” Sijui.”

Borussia Monchengladbach wameonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji namba mbili wa Tottenham, Vincent Janssen kwa mujibu wa taarifa kutoka jarida la Bild.

Mdachi huyo ameshindwa kufanya vizuri katika msimu wake wa kwanza katika ligi kuu ya Uingereza na klabu hiyo ya Ujerumani ipo tayari kutoa kiasi cha pauni milioni 12 na kupata huduma yake.

Lyon wametangaza usajili wa straika Mariano Diaz, kutoka Real Madrid. Mariano anakuwa usajili wa nne kwa Lyon majira haya ya kiangazi. Je usajili huu ni ishara kwamba wapo tayari kumuuza Lacazette.
By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents