Michezo

USAJILI: Niyonzima bado anamkataba na Yanga – Mkwasa

Mara baada ya dirisha la usajili kufumguliwa rasmi kumekuwa na mvutano mkubwa kwa baadhi ya majina makubwa ya wachezaji kuhusishwa kuhamia katika timu mbali mbali miongoni mwa majina ambayo yanaonekana kuteka vyombo vya habari katika kipindi hiki ni lile la kiungo wa klabu ya Yanga SC na Timu ya Taifa ya Rwanda, Haruna Niyonzima.

Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa

Kufuatia hilo Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa amewatoa hofu wanachama na mashabiki wa Yanga juu kiuongo wao Haruna Niyonzima ameyazungumza hayo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram wa klabu hiyo

“Masuala ya Haruna nafikiri eeh pia niseme kama suala lake linafanana na masuala mengine yote ya usajili Haruna bado ni mchezaji wetu na mkataba wake bado haujamalizika”.

“Na natambua kwamba tayari tushampa taarifa ya kumalizana naye na kuzungumza naye katika masuala mazima ya usajili wake”.

Kiungo wa klabu ya Yanga SC na Timu ya Taifa ya Rwanda, Haruna Niyonzima

“Nafikiri yeye aliaga hapa alienda kwenye National team, ninavyo fahamu mimi ameenda kwenye national team na ameahidi kurudi hapa tarehe 13 na atakapo rudi tutaendelea na mazungumzo naye”. Alisema Mkwasa ambaye ni Katibu Mkuu wa Klabu.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents