Usalama majini umeboreswa

Pichani kutoka kulia: Mkurugenzi wa Sumatra Israel Sekirasa, Waziri wa Miundombinu Dkt.Shukuru Kawambwa, Katibu Mkuu wa IMO Efthimios Mitropoulos, Meneja wa Bandari Jason Rugaihuruza.
Pichani kutoka kulia: Mkurugenzi wa Sumatra Israel Sekirasa,Waziri wa Miundombinu Dkt.Shukuru Kawambwa, Katibu Mkuu wa IMO Efthimios Mitropoulos, Meneja wa Bandari Jason Rugaihuruza.

Waziri wa Miundombinu Dkt.Shukuru Kawambwa amemshukuru Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Majini (IMO) Efthimios Mitropoulos kwa kuiwezesha Tanzania kufanikisha upatikanaji wa mitambo maalumu itakayosaidia usalama pindi vyombo husika vya safari majini viwapo safarini.


Mitambo hiyo  iliyogharimu kiasi cha shilingi zaidi ya Sh.150 milioni
za kitanzania pamoja na gharama zingine ambazo zitatumika katika kutoa
mafunzo  ya kitaalamu kwa baadhi ya wafanyakazi juu ya namna ya
kuiendesha na kuisimamia
mitambo hiyo.

Kawambwa amesema kuwa kupatikana kwa mitambo hiyo kutaiwezesha nchi
yetu kupiga hatua kubwa katika suala zima la usalama wa majini ambapo
kwa miaka mingi tatizo la usalama wa majini limekuwa la wasiwasi huku
mawasiliano yakiwa ndiyo kikwazo kikubwa cha kuhakikisha usalama wa
vyombo hivyo pindi viwapo safarini au katika shughuli zingine za
kiuvuvi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents